BENITEZ KUWAPANGA PAMOJA TORRES NA DEMBA BA
Demba Ba
Fernando Torres
By Salim
"Wanaweza kucheza
pamoja safu ya mbele ya Chelsea. Ba alikuwa akicheza akiwa na Papiss Cisse
katika kikosi cha Newcastle, hivyo yeye anaweza kabisa kucheza ushambuliaji
pacha"
KOCHA Rafael Benitez
amesema haoni sababu kwa nini washambuliaji wake Demba Ba na Fernando Torres
wasiwezer kucheza pamoja kwa mafanikio, kauli aliyopitoa baada ya Ba kufunga
mara mbili katiika mechi yake ya kwanza tangu ajiunge
Chelsea.
Ba, juzi lifunga mara
mbili katika pambano la raundi ya tatu ya Kombe la FA, kuiwezesha Chelsea
kuiondosha mashindanoni Southampton, kwa mabao 5-1 mechi iliyochezwa kwenye
Uwanja wa St Mary’s.
Huku Torres akianzia
benchi katika mechi hiyo ya Jumamosi, Ba ilimchukua takribani dakika 35 kufunga
bao lake la kwanza kabisa akiwa na Chelsea, ambalo lilikuwa la kusawazisha na
kufungua mvua ya mabao baadaye.
"Wanaweza kucheza
pamoja safu ya mbele ya Chelsea," alisema Benitez baada ya mechi
hiyo.
"Ba alikuwa akicheza
akiwa na Papiss Cisse katika kikosi cha Newcastle, hivyo yeye anaweza kabisa
kucheza ushambuliaji pacha na mwenzake kwa sababu ni mchezaji mjanja, lakinipia
inategea na mfumo wa mchezo na nyota anaoshirikiana nao.
"Napendelea tatizo
hili la kuwa na washambuliaji wawili, kuliko kupaswa kuwa na mmoja anayetakiwa
kuwa makini mchezoni kwa dakika zote.
"Jambo muhimu kwa timu
ni kuwa na wigo mpana wa uteuzi wa kikosi. Wao ni wachezaji wazuru na kimsingi
wanaweza kupambana, au labda tunaweza kuwaongoza wao pamoja – inategemea na
mchezo."
Ba alifunga bao moja
katika kila kipindi, katika mechi ambayo kulikuwa na mabao kutoka kwa Victor
Moses, Branislav Ivanovic na penati ya dakika za lala salama ya Frank
Lampard.
"Ni muhimu mno kwa
mshmabuliaji kufunga mabao, mengi zaidi awezavyo, lakini zaidi ni kwana nmna
gani ushirikiano wake na timu unakuwa na uelewa alionao katika kuweza kutambua
nini tunatarajia ambavyo vyote vimeniridhisha," alisema
Benitez.
"Alionesha uzuri wake
mbele ya lango na kila alichofanya dimbani katika mechi hii kilinivutia na
kuniridhisha vya kutosha. Alikuwa mjanja mno mchezoni."
Aidha, bao la mtokea
benchi Lampard katika mechi hiyo, lilimfanya aifikie rekodi ya utikisaji nyavu
mara nyingi zaidi katika klabu hiyo kwa kufikisha mabao 193 na kumpiku mshikilia
rekodi hiyo wa kudumu Kerry Dixon anayeshika nafasi ya pili
sasa.
No comments:
Post a Comment