coming soon

coming soon

Thursday, January 10, 2013

R.I.P OMARI OMARI WA MAJALIWA....



MSANII nyota wa miondoko ya Mnanda 'Mchiriku', Omar Omar, amefariki dunia usiku wa kuamkia jana baada ya kuugua kwa muda mrefu. Omar Omar aliyetamba na nyimbo mbalimbali ukiwemo ule maarufu wa 'Kupata ni Majaliwa'

Wednesday, January 9, 2013

BONGO MOVIE NA BONGO FLEVA SIYO - KITALE.

Mussa Yusuf
                               Kitale Komediani kutoka Swahiliwood      
 
 
 
MWIGIZAJI wa filamu na Komedi Mussa Yusuf ‘Kitale’ amaewashukia wasanii wa filamu na muziki wa kizazi kipya Bongo fleva kwa kusema ni wanafiki hawana urafiki wa ukweli kati yao msanii huyo alisema hayo kufuatia kuzorota kwa arobaini ya rafiki yake kipenzi marehemu Hussein Mkiety ‘Sharomilionea’ kuhudhuriwa na wasanii wachache na kuchangiwa na watu watano tu.

Hussein Mkiety
Marehemu Sharomilionea enzi za uhai wake.
 
Mussa Yusuf
                                  Kitale akiwa katika pozi.

Tuesday, January 8, 2013

BENITEZ KUWAPANGA PAMOJA TORRES NA DEMBA BA



Demba Ba
 
Fernando Torres

By Salim
"Wanaweza kucheza pamoja safu ya mbele ya Chelsea. Ba alikuwa akicheza akiwa na Papiss Cisse katika kikosi cha Newcastle, hivyo yeye anaweza kabisa kucheza ushambuliaji pacha"

KOCHA Rafael Benitez amesema haoni sababu kwa nini washambuliaji wake Demba Ba na Fernando Torres wasiwezer kucheza pamoja kwa mafanikio, kauli aliyopitoa baada ya Ba kufunga mara mbili katiika mechi yake ya kwanza tangu ajiunge Chelsea.

Ba, juzi lifunga mara mbili katika pambano la raundi ya tatu ya Kombe la FA, kuiwezesha Chelsea kuiondosha mashindanoni Southampton, kwa mabao 5-1 mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa St Mary’s.

Huku Torres akianzia benchi katika mechi hiyo ya Jumamosi, Ba ilimchukua takribani dakika 35 kufunga bao lake la kwanza kabisa akiwa na Chelsea, ambalo lilikuwa la kusawazisha na kufungua mvua ya mabao baadaye.

"Wanaweza kucheza pamoja safu ya mbele ya Chelsea," alisema Benitez baada ya mechi hiyo.

"Ba alikuwa akicheza akiwa na Papiss Cisse katika kikosi cha Newcastle, hivyo yeye anaweza kabisa kucheza ushambuliaji pacha na mwenzake kwa sababu ni mchezaji mjanja, lakinipia inategea na mfumo wa mchezo na nyota anaoshirikiana nao.

"Napendelea tatizo hili la kuwa na washambuliaji wawili, kuliko kupaswa kuwa na mmoja anayetakiwa kuwa makini mchezoni kwa dakika zote.

"Jambo muhimu kwa timu ni kuwa na wigo mpana wa uteuzi wa kikosi. Wao ni wachezaji wazuru na kimsingi wanaweza kupambana, au labda tunaweza kuwaongoza wao pamoja – inategemea na mchezo."

Ba alifunga bao moja katika kila kipindi, katika mechi ambayo kulikuwa na mabao kutoka kwa Victor Moses, Branislav Ivanovic na penati ya dakika za lala salama ya Frank Lampard.

"Ni muhimu mno kwa mshmabuliaji kufunga mabao, mengi zaidi awezavyo, lakini zaidi ni kwana nmna gani ushirikiano wake na timu unakuwa na uelewa alionao katika kuweza kutambua nini tunatarajia ambavyo vyote vimeniridhisha," alisema Benitez.

"Alionesha uzuri wake mbele ya lango na kila alichofanya dimbani katika mechi hii kilinivutia na kuniridhisha vya kutosha. Alikuwa mjanja mno mchezoni."

Aidha, bao la mtokea benchi Lampard katika mechi hiyo, lilimfanya aifikie rekodi ya utikisaji nyavu mara nyingi zaidi katika klabu hiyo kwa kufikisha mabao 193 na kumpiku mshikilia rekodi hiyo wa kudumu Kerry Dixon anayeshika nafasi ya pili sasa.

 PRINCESS YA WOLPER KUTOKA HIVI KARIBUNI



Nyota wa filamu nchini, Jacline Wolper anajipanga kusambaza kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Princess’, hivi karibuni.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Wolper alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kazi hiyo ambayo anamini itakuwa gumzo mtaani kutokana na stori ambayo ameielezea ndani yake.

Alisema anawaomba wadau wa kazi zake wakae mkao wa kula kwaajili ya kazi hiyo ambayo anatarajia kuisambaza hivi karibuni.

“Namshukuru mungu maandalizi ya kazi yangu yameenda vizuri na hadi sasa ndio namalizia kazi hii, wapenzi wa kazi zangu wake vizuri kwaajili ya kuipokea kazi hii ambayo imefuata maadili ya mtoto wa kitanzania,” alisema Wolper.

Alisema yeye ni Mtanzania hivyo ameamua kufanya kitu ambacho kipo katika jamii inayomzunguka na kuelimisha kwa uwezo aliokuwa nao yeye.

Ayew aachwa nje ya kikosi cha Ghana

 
 
Andre Ayew

UBOVU HUU WA BARABARA NI USALITI WA SPIKA MAKINDA KWA WAPIGA KURA WAKE

 
                           Barabara za jimboni kwa spika Makinda kama zinavyoonekana
Magari yakipita kwa shida katika barabara za jimboni kwa Makinda barabara ya Njombe -Ludewa maeneo ya Uwemba

 
Spika Makinda siku alipoapa kuwatumikia wananchi wa jimbo la Njombe kusini

UBOVU huu wa barabara ya Njombe - Ludewa katika jimbo la Njombe kusini mkoa mpya wa Njombe jimbo linaloongozwa na spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Anne Makinda ni usaliti mkubwa kwa wapiga kura .

Nalazimika kusema kutumia kauli ya usaliti kutokana na kipindi kirefu cha miaka 40 ya ubunge wa Mheshimiwa Makinda katika jimbo hilo na hali halisi ya uchakavu wa miundo mbinu katika jimbo lake hilo.

Mbali ya kuwa spika hawezi kutumia nafasi yake kuuliza swali bungeni juu ya ubovu huo wa barabara ila anayonafasi ya kutumia njia mbadala ya kufikisha kilio cha wananchi wa jimbo hilo juu ya ubovu huo wa miundo mbinu .

Kwani mtazamo wa wageni wanaoingia na kutoka katika jimbo hilo na wapiga kura wa jimbo hilo ni ule wa kufikiri kuwa mbunge wao Makinda amelitelekeza jimbo hilo kwa kujitoa kuwa mwalilishi wao bungeni .

Kwa wenyeji wa jimbo hilo la Njombe kusini na wale wa jimbo la Ludewa wanaweza kuwa mashahidi wazuri wa kero hii ya miundo mbinu katika jimbo la Njombe kusini na iliyopo jimbo la Ludewa.

Hakuna asiyetambua kuwa ukitoka njiapanda ya Songea kuingia barabara ya mvumbi kijiji cha Nundu hadi Luponde barabara yake ni chafu kupita kiasi na ndicho Kipande ambacho wasafiri hukwama na hata vyombo vya usafiri huharibika kutokana na Kipande hicho ambacho kwa madereva hutumia zaidi ya saa moja kupita eneo hilo huku baadhi ya magari hulazimika kulala eneo hilo kusubiri huruma ya mwenyezi Mungu ya kuleta jua ili kuweza kupita vinginevyo kupita hapo ni sawa na ndoto za alinacha .

Hivyo kutokana na ubovu wa Kipande hicho cha Nundu - Luponde katika jimbo hilo la Njombe kusini na uzuri wa miundo mbinu ya Kuanzia mpakani mwa jimbo la Niombe na Ludewa ni wazi waweza kuungana nani kuwa Spika Makinda ameamua kuwasaliti wapiga kura wake na kutumia miaka 40 ya ubunge wake kwa kuwaacha wapiga kura katika maswali mengi zaidi kuliko majibu .

Hivi ni nani asiyetambua kuwa wapiga kura wa jimbo la Njombe kusini ni miongoni mwa wapiga kura wenye bahati kubwa kwa mbunge wao kuendelea kuwa chaguo la Taifa kwa kushika nafasi kubwa za kitaifa ikiwa ni pamoja na kuwa naibu spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika uongozi wa spika Samweli Sitta na katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 wananchi wa jimbo hilo waliweza kujenga Imani kubwa ya kumchagua tena na wabunge kujenga matumaini makubwa na kumchagua kuwa spika wa kwanza Mwanamke na kuweka historia ndani ya nchi na barani Afrika Kama si duniani.

Sipendi kwa leo kuhusiana utendaji wake Kama spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania na uwakilishi wake kama mbunge wa jimbo la Njombe kusini ,japo hakuna asiyetambua kuwa Kati ya ma spika walioonyesha kupwaya kukikalia kiti hicho cha uspika na Kama utatakiwa kuwataja kwa majina basi ni vigumu kuliacha kulitaja jina la Mheshimiwa Anne Simamba Makinda mbunge wa jimbo la Njombe kusini.

Pamoja na kuwa mapungufu ni kawaida kwa kiongozi awaye yeyote yule ila yapo mapungufu mengine ambayo ni aibu kwa kiongozi moja ya mambo yanayoweza kumpa kiongozi aibu na kuchokwa zaidi na wale anaowaongoza kwa kero Kama hizi za miundo mbinu Kwani unapozungumzia maendeleo ya jimbo na wananchi ni vigumu kuacha kuangalia usalama wa miundo mbinu ,Elimu ,chakula ,afya ya wale unaowaongoza .

Hivyo Kama kiongozi mwakilishi wa wananchi umeshindwa kuwatetea ama kusimamia ujenzi wa miundo mbinu bora na kuacha eneo Lake analoliongoza bila kuwa na miundo mbinu mizuri ni wazi hakuta kuwa na maendeleo na usalama wa chakula ,afya na Elimu utaendelea kuwa mashakani zaidi.

Kwa upande wa jimbo la Njombe na wilaya nzima ya Njombe ni moja Kati ya maeneo ambayo wananchi wake wanategemea zaidi kilimo hivyo kuendelea kuiacha miundo mbinu ambayo ni barabara bila kutegeneza ni wazi ni kuwakomoa wananchi hao ambao wanategemea miundo mbinu kamili ili kujikwamua katika dimbwi la umasikini.

Ikumbukwe kuwa hii ni miaka 50 sasa toka nchi yetu ilivyopata Uhuru wake mwaka 1961 hivyo ilipaswa kuwa ni matumaini Mapya Kwa waanchi wa pembezoni mwa Tanzania kuona miundo mbinu bora inakuwepo katika maeneo Yao na hata ikiwasaidia kuona jitihada za ujenzi wa barabara za lami katika maeneo Yao.

Leo ni aibu kwa Taifa kuona wilaya Kama Njombe,Ludewa na Mufindi hazi barabara za lami wakati katika maeneo hayo yamekuwa yakiongoza kusaidia uchumi wa Taifa kukua zaidi.


Wakizungumzia hali hiyo ya ubovu wa barabara katika barabara jimbo la spika Makinda wananchi wa kijiji cha Nundu na Luponde walisema kuwa eneo hilo la Nundu na Luponde ambalo limekuwa likisumbua zaidi kipindi cha masika na hata kupelekea mabasi ya abiria kukwama lina urefu wa takribani Kilometa 63 ambazo mabasi hutumia muda wa zaidi ya masaa matatu badala ya dakika 30 hadi 45 Kama ilivyo lami

Yohana Sanga ambaye ni mkazi wa kijiji cha Luponde alisema kuwa ubovu wa barabara hiyo iliyopo jimboni kwa spika wa bunge imekuwa ni kero kubwa na hata kupelekwa wananchi kuendelea kujenga chuki na serikali ya CCM na mbunge huyo kwa kushindwa kuimaliza kero hiyo.

Sanga alisema kuwa kutokana na kero hiyo ya ubovu wa barabara wapinzani wameendelea kuliteka jimbo hilo la Njombe kusini na kuweka ngome yao kwa madai kuwa mbunge wao spika Makinda amelitelekeza jimbo hilo .

Kwani alisema kuwa haiwezekani jimbo hilo kuendelea kuwa na barabara mbovu Kama hiyo wakati Mbunge wao ni mmoja Kati ya viongozi wakubwa nchini na walitegemea nafasi yake katika Taifa kuwa ni sehemu ya ufumbuzi wa kero za miundo mbinu inayowakabili wananchi wa jimbo la Njombe kusini.

Makinda amekuwa mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa akitokea Njombe na amekuwa mbunge kamili wa jimbo toka mwaka 1995 hadi sasa na amepata kushika nafasi ya unaibu spika na uspika kamili mwaka 2010 ila bado ameshindwa kutumia vema nafasi yake Kama mwakilishi wa wananchi wa jimbo la Njombe kusini wala kutumia heshima ya uspika kuelekeza maendeleo jimboni kwake.

Katakana na uwajibikaji mbovu wa Makinda kwa wapiga kura wake imekuwa ni mwanzo wa jimbo la Njombe kusini kuwa ngome ya Vyama vya upinzani hasa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) ambacho kimefanikiwa kuwa na idadi kubwa ya wanachama na mashabiki katika jimbo hilo huku bendera za CCM zikishushwa na kuwekwa za Chadema.

Japo sina uhakika kuwa wote wameamua kuhama CCM katakana na uwajibikaji mbovu wa mbunge wao ila Kama wahenge walivyonena kuwa dalili za mvua ni mawingu basi tuchukulie haya ni mawingu Makinda na CCM yake wajiandaa kwa miamvuli ili kujihamia na mvua Kali .

Dalili za mbunge kushindwa katika uwakilishi wake kwa wananchi zipo Nyingi moja ni utendaji na kauli zake na pili mtazamo wake na wananchi dhidi yake ambapo mtazamo wa Makinda mwenyewe kwa wapiga kura wake ni huu wa kuwachukulia wapiga kura Kama ni watu wanaotegemea kuomba Pesa Kutoka kwake hadi kufikia hatua ya kuwakimbia na kuwalalamikia katika vikao vya Chama kuwa wapiga kura omba omba ambao kila wakimwona wanataka Pesa.

Sitaki kumwagiza spika wangu Makinda kuwaomba radhi wapiga kura wake kwa kuwaita omba omba ila namwangukia na kumlamba miguu kumwomba kutorudia tena kauli Kama hiyoaliyoitoa katika kikao cha kwanza cha Halmashauri kuu ya Chama cha mapinduzi( CCM) kilichohudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo wabunge wote wa mkoa wa Njombe Kama Deo Filikunjombe, Dr Binilith Mahenge, Deo Sanga, Gyerson Lwenge ,Pindi Chana na Lediana Mng,ong,o na makanda wa CCM.

Hivi hebu tujiulize Leo Makinda ambae ameongoza jimbo hilo toka mwaka 1995 hadi sasa Kama Vipindi vinne sasa ameshindwaje kufanya japo kitu kimoja cha kuonekana na kusingizia Pesa hakuna wakati jirani yake mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe kwa Kipindi chake cha kwanza tu ameanza kuonyesha mafanikio Makubwa Ludewa hata kuweka historia ya Karne kwa kuanza ujenzi wa lami Ludewa ambayo haijapata kuwepo toka nchi ipate uhuru wake mwaka 1961? Ni vema CCM kuacha kuwachukia wanachama wanaofanya vema na kusema ukweli kuwa nimaadui na kuendelea kuwakumbatia wabunge Kama Makinda kuwa ni wema huku wapiga kura wakiwaona Kama ni maadui hivyo ili nchi iweze kusonga mbele katika maendeleo ni lazima wabunge Kama akina Makinda tukawapumzisha pembeni na kuweka wabunge watendaji
Lionel Messi avunja rekodi ya kuwa mchezaji bora wa Dunia mara Nne    mfululizo. ( 2009, 2010, 2011, 2012).
Ronaldo achukua nafasi ya pili na Iniesta achukua nafasi ya tatu.
Hongera kwa Lionel Messi.
 
 
Lionel Messi avunja rekodi ya kuwa mchezaji bora wa Dunia mara Nne mfululizo. ( 2009, 2010, 2011, 2012).
Ronaldo achukua nafasi ya pili na Iniesta achukua nafasi ya tatu.
Hongera kwa Lionel Messi.