Mrembo huyo ni Miss Akuot Philip Suzan (20) mwenye urefu wa futi
6.1 anaekaa Juba, Sudan ni mwanamitindo nchini humo na anatarajia
kujiunga na Chuo Kikuu Cha Makerere Nchini Uganda mwaka huu.
Warembo ambao tayari wameshapatikana kutoka katika Nchi mbalimbali
kwa ajili ya mashindano hayo ni mwakilishi wa Eritrea: Miss Rahwa
Afeworki (22), kutoka Ethiopia ni: Miss Lula Teklehaimanot (19) na Miss
Ayisha Nagudi (23) ambae ni mwakilishi wa Uganda.
Nchi zilizobaki zinaendelea kutafuta wawakilishi watakaoziwakilisha
Nchi zao katika mashindano ya Miss East Africa 2012 ambayo
yatazishirikisha Nchi 16 za ukanda huu ambazo ni Tanzania (wenyeji),
Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine ni Southern Sudan,
Somalia, Djibouti, Eritrea, Ethiopia pamoja na visiwa vya Mauritius,
Madagascar, Comoros, Reunion na Seychelles.
Mashindano ya Miss East Africa ndio mashindano makubwa ya urembo kwa ukanda huu wa Africa.
Fainali za mashindano ya Miss East Africa ambazo huandaliwa na
kumilikiwa na Kampuni ya Rena Events Ltd, zitafanyika tarehe 07 mwezi
September mwaka huu jijini Dar es salaam, Tanzania
No comments:
Post a Comment