WAETHIOPIA KUCHEZESHA YANGA, ZAMALEK
Waamuzi kutoka Ethiopia ndiyo
watakaochezesha mechi namba 7 ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na
Zamalek ya Misri itakayochezwa Februari 18 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika
(CAF) limemteua Bamlack Tessema kuwa mwamuzi wa kati kwenye mechi hiyo wakati
waamuzi wasaidizi ni Yilma Knife na Mussie Kindie. Mwamuzi wa akiba (fourth
official) atakuwa Waziri Sheha wa Tanzania na Kamishna wa mchezo huo ni Charles
Kafatia wa Malawi.