coming soon

coming soon

Wednesday, November 28, 2012

STAR TV YAIBUA TUHUMA NZITO ZA NGONO KATIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA ( UDOM)

Taarifa ya habari ya Star tv ya saa mbili usiku ya tarehe 23/11/2012 imeeleza kuwa wanafunzi wa kike katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wanadaiwa kufanya biashara ya ukahaba katika maeneo mbalimbali ya starehe mjini Dodoma!

Habari hii inasikitisha hasa ukizingatia umuhimu wa wasomi hawa katika Tanzania na hatari inayoweza kuwapata kama taarifa hii ina ukweli.

Kama jamii tujiulize, tatizo ni nini mpaka mtu wa level kama hiyo kuamua kuvaa vichupi na kujiuza kwenye clubs na sehemu zingine??

CHUO KIKUU cha Dodoma UDOM kinadaiwa kukumbwa na kashfa ya ngono kufuatia madai kwamba baadhi ya wananafunzi wa kike wanajihusisha na biashara ya kuuza miili yao kwa lengo la kujikimu kimaisha.

Tuhuma hizo zimebainika wakati wa mahafali ya tatu ya UDOM huku takribani wahitimu 6392 wakitunukiwa vyeti,stashahada,shahada za kwanza,uzamili na shahada za uzamivu.

Chuo Kikuucha Dodoma ambacho kilianzishwa rasmi mwezi machi mwaka 2007 kimejipatia sifa kemkekm za kitaaluma licha ya ukweli kwamba bado ni kigeni machoni pa wengi.

Tuhuma za ngono miongoni mwa wanafunzi wa kike zinadaiwa kusababishwa na ukata hatua inayowalazimu kutoroka chuoni nyakati za usiku na kujiunga na baadhi ya wasichana wa mitaani waliokubuhu kwenye ukahaba maarufu kama machangudoa kwa lengo la kujiuza.

Wakizungumza na star tv wakati wa mahafali hayo baadhi ya wahitimu wanathibitisha uwepo wa vitendo hivyo vilivyo kinyume na maadili.

Kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof.Idris Kikula anatoa onyo kali kwa wote watakaobainika.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amenukuliwa kwa nyakati tofauti akisisitiza suala la maadili chuoni hapo hatua inayodaiwa kupuuzwa na wanaojihusisha na vitendo hivyo.

AUDIO: KAMANDA WA POLISI TANGA ATOA UFAFANUZI KUHUSU KIFO CHA SHARO MILIONEA

Namkariri Kamanda wa Polisi Tanga akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo la Maguzonizonga wilayani Muheza hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”

Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei

WASANII WATOA NYIMBO MBILI ZA HUZUNI SANA WAKIMLILIA MSANII SHARO MILIONEA....

DOWNLOAD WIMBO HUU WA MAOMBOLEZO

Tunda Man ft. Mirror & Raymond - R.I.P Sharomilioner

Huu ni wimbo ambao kiukweli umenitoa machozi

Huu chini ni Wimbo ambao umefanywa na producer monagangstar....

Waliofanya hii ngoma ni DOGO JANJA,PNC KUTOKA MTANASHATI/.OSTAZ JUMA NAMUSOMA) ,STAMINA,COUNTRY BOY MTU CHEE,NAY WA MITEGO,SAPRANO,SUMA MNAZALETI,ELLY NIZO,BRIGHT,MAKOMANDO WAZEE WA KIBEGA,N,K

DOWNLOAD WIMBO HUU.NI WIMBO WA MAOMBOLEZO
 
TASWIRA MBALIMBALI ZA GARI ALILOPATA NALO AJALI MSANII SHARO MILIONEA NA JINSI UMATI WA WANANCHI ULIVYOFURIKA NJE YA CHUMBA CHA MAITI HOSPITALI TEULE YA MUHEZA

Gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.
Baadhi ya watu wakiliangalia gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.

Gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.
Mbunge wa Jimbo la Muheza Hebert Mtangi akiwasili nje ya jengo la Chumba cha Kuhifadhia Maiti cha Hospitali ya Teule Muheza kwa ajili ya kushuhudia mwili wa msaniii Sharo Millionea aliyekufa katika ajali ya gari wakati akitoka Dar es Salaam kwenda Lusanga, Muheza mkoani Tanga, ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Kijiji cha Songa Kibaoni .
Wakazi wa wilaya ya Muheza na maeneo mengine wakiwa wamefurika nje ya Chumba cha Maiti cha Hospitali Teule Muheza, kusubiri kushuhudia mwili wa Sharo Millionea, aliyefariki kwa ajali ya gari